
Stergomena Tax akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia. Dk.Tax ameishukuru Jamhuri ya Namibia kwa ushirikiano ilioutoa katika hatua za kuanzisha ubalozi huo na uwepo wao katika tukio hilo muhimu na la kihistoria kwa nchi hizo mbili.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Dk Modestus Kipilimba (kushoto) wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi za Ubalozi jijini Windhoek, Namibia.

