NA MWANDISHI WETU
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Marekani, limemuita Mtanzanja Bernard Kamungo kuitumikia timu ya mpira wa miguu ya taifa hilo.
Kamungo ambaye ni Mtanzania aliyezaliwa na kukulia Kasulu mkoani Kigoma alihamia Marekani na wazazi wake mwaka 2016 akiwa na miaka 14
Kinda huyo anayekipiga kwenye klabu ya FC Dallas ya Marekani inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo (MLS League ) ameitwa kuchezea timu ya raifa ya Marekani kwenye orodha iliyotajwa Oktoba 8 mwaka huu.
Orodha hiyo ni ya kikosi cha Marekani kwa wachezaji walio chini ya miaka 23 watakaokwenda kushiriki mashindano ya Olympic ya mwaka 2024.
Kamungo aliitwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Juni 2023 iliyokuwa inajisndaa na mchezo dhidi ya Niger lakini hakucheza kwa kile kilichoelezwa kuwa ni changamoto ya Pasi ya Kusafiria ya Tanzania.
Kamungo anatakiwa kuonesha uwezo wa juu ili kupata nafasi katika orodha ya mwisho ya kikosi kitakachoiwakilisha Marekani