NA MWANDISHI WETU
Chuo Kikuu cha Jawarhalal Nehru, Delhi cha nchini India kimemtunuku PhD Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 10, 2023
Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) ametunukiwa kwa mchango wake kwenye diplomasia ya uchumi, maendeleo yanayogusa wananchi moja kwa moja na mchango wake kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
Mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Samia ameitunuku kwa mabinti wa Tanzania wanaoishi katika mazingira magumu akiwataka wajitume na kujitoa kwa moyo wao wote wanapigekeleza majukumu yao.
Tangu alipoingia madarakani, Rais Samia ameweka jitihada kusaidia watoto wakike ikiwa ni pamoja na kuruhusu wanafunzi waliojifungua kurejea shule na kuendelea na masomo.
Hii ni shahada ya kwanza ya udaktari kwa Rais Samia kutunukiwa ugenini na ya kwanza kutolewa kwa mwanamke na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru.