NA MWANDISHI WETU,DODOMA



MKURUGENZI wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Ramadhani Kailima leo Agosti 30, 2025 ameongoza kikao cha Wawakilishi wa Vyama vya Siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.


Mikutano hiyo iliyoanza Agosti 28, 2025 inaendelea hadi Oktoba 28, 2025 kwa Tanzania Bara na Oktoba 27, 2025 kwa Tanzania Zanzibar.

Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika Oktoba 29, 2025.



