NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WADAU mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikalini wameshiriki kwenye kikao cha mazungumzo yaliyoandaliwa na Shirika la ToastMasters International ambacho kimeanza Mei 19,2023 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Mei 19,2023 jijini Dar es Salaam baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho cha siku ya kwanza cha ToastMasters ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Afrika Mashariki na hasa Tanzania, Kiongozi wa ToastMasters Kanda ya Mashariki Emilia Siwingwa amesema wameanza vikao vya mkutano mkuu wa mwaka na utaendelea kwa siku mbili.
“Katika kikao chetu cha kwanza ambacho tumeshirikisha wadau kutoka sekta binafsi pamoja na serikali sambamba na wanachama wetu wa Afrika Mashariki, mengi tumezungumza kwa lengo la kuhakikisha tuaendelea kuboresha sekta ya biashara na uwekezaji.
“Tumezungumza na kujadiliana kwa kina na miongoni mwa mambo ambayo tumeyaangali ni je tunafanya maendeleoe endelevu? Je kwenye uwekezaji tuko wapi lakini pia tukiangalia na upande wa biashara.Katika maeneo yote lazima unamuangalia mwanadamu, je anauwezo gani, ana ujuzi gani wa kuweza kuhakikisha maendeleo yanatekelezwa.”
Akifafanua zaidi amesema yeye ni Wakili wa kujitegemea lakini alichobaini huwezi kuendelea bila kuwa na uwezo wa kujielezea , kuwasiliana na watu ili ukisema wanakuelewa na wewe ukisikia kitu unakielewa , hivyo kwenye mazungumzi ya leo wamejadili kwa kina mambo hayo.
Pamoja na mambo mengine, amesema wametoka na mikakati mipya ambapo wamekubaliana kwamba iko haya ya kuendelea kuzungumza na kushirikisha Serikali katika masuala yanayowezesha kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji sambamba na kusaidia jamii kuwa na maendeleo.
“Tumekubaliana haya mazungumzo lazima yaendelee kwani yanagusa maslahi ya wanadamu,kwa hiyo tumekubaliana tuendelee kuzungumza , tuilete Serikali karibu ili tuweze kufikia mikakati itakayoweza kusaidia wananchi.
“Katika ya sekta ya biashara , katika sekta ya uwekezaji, huwezi kupata mafanikio , huwezi kuboresha sekta ya biashara bila kuna na watu ambao wanapata uelewa zaidi , kwa hiyo leo tulikuwa na watalaamu mbalimbali ambao wametusaidia kutungea uelewa zaidi na hivyo tulivyokuja ni tofauti na tulivyoondoka.”
Kuhusu wanachama wa ToastMasters nchini Tanzania amesema idadi yao sio kubwa ukilinganisha na nchi kama Kenya lakini wamebaini huenda hakujakuwa na hamasa kubwa zaidi lakini kupitia kikao cha leo kuna idadi kubwa ya watu wameomba kujiunga, hivyo matarajio yao wataendelea kuongezeka siku hadi siku.