NA MWANDISHI WETU, TANGA
KATIKA kuunga mkono Serikali ya Awamu Sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan Benki ya NMB imekuwa ikitoa zaidi ya Bilioni 60 /-kila mwezi kwa ajili wa wajasiriamali wadogo wadogo hapa nchini ili kuwawezesha waweze kujikwamua kiuchumi na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe,wakati kikao cha wafanyabiashara mbalimbali mkoani Tanga wanaohudumiwa na Benki hiyo.
Changarawe amesema kwamba hatua hiyo imewajengea uzoefu mkubwa namna ya kuwahudumia wajasiriamali hao na kutokana na utoaji wa mikopo hiyo umewawezesha kuongeza nguvu kwenye mitaji yao na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.
“Hapa Tanga tulikutana na wateja kuwaambia kitu gani wamekianzisha na wakifanye ili kuweza kuboresha huduma zao kwa sasa wana huduma waliyoanzisha kwa ajili ya wateja wanaofanya huduma kwenye masoko yanayosimamiwa vizuri na serikali yana vizimba na wateja wameandikishwa”amesema
Amesema kwamba ili kuhakikisha nao wananufaika na mikopo hiyo wameanza kutoa mikopo kuanzia 100,000 hadi 1000000 bila dhamana na baadaye 1, 000, 000 hadi 2, 000, 000 iwapo mteja anaweka dhamana na wana mikopo mengine zaidi ya hapo inakwenda hadi 5, 000, 000 kwa wateja wao.
“Pia tumeanzisha mikopo kwa ajili ya vijana wanaojihusisha na bodaboda ambapo kitu ambacho kinahitajika ni kujiandikisha kwenye vyama vyao ambavyo vinatambulika na serikali na yeye ni kutafuta asilimia 20 ya chombo anachokitaka akishapata benki inaongzekja kiasi kilichobaki ili kumpatia”amesema Meneja Mwandamizi wa mikopo NMB Makao Makuu.
Hata hivyo amesema kwamba baadaye wanafanya biashara na kufanya marejesho kila wiki kumaliza deni kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 hadi watakapoikamilisha ili kuwezesha na wengine kunufaika nayo.
Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB-Praygod Godwin amesema kwamba wamekutana na wafanyabiashara kuweza kutengeneza mtandao na kubadilishana uzoefu ikiwemo kuwapa mafunzo ya vitu mbalimbali na mwaka huu wamewafundisha vitu vitatu.
Amesema kikao hicho kilikuwa ni mahususi kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwaeleza mteja anatakiwa kuangalia
“Mfano anafanyabiashara ya usafirishaji anatumia petrol lakini dunia inabadilika magari mengi yanabadilika kwenye matumizi ya gesi na mama lishe anatumia mkaa lakini dunia ya leo wanatoka kwenye mkaa kwenda kwenye gesi hivyo watawafundisha mbinu mbalimbali na mambo ya kurekodi taarifa za mapato na matumizi na umuhimu wake”
Hata hivyo alisema pia wataalamu hao watawafundisha jinsi mfanyabiashara kuangaa ikitokea amepata changamoto za kiafya,uzee nani atasimamia biashara zake pia wataangalia namna ya kuwafudnisha katika mambo hayo muhimu.
Katika kikao hicho kiliwakutanisha wafanyabiashara 150 wa mkoa wa Tanga wenye matawi 12 kwa mkoa ambapo inaelezwa kwamba kitakuwa na tija kwa siku zijazo katika kuendeleza biashara zao na hatimaye kukuza mtaji wao.
Naye kwa upande wake Mfanyaabiashara Celina Ndumbaro alisema kwamba alichojifunza katika mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuweza kuona namna ya kufanya biashara zao kwa tija na kuweza kupata mafanikio.