NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya Simba SC, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) kwa kishindo baada ya kuibamiza Ihefu Fc kwa mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar Salaam leo Aprili 7, 2023
Simba ilifanikiwa kupata mabao 4 katika kipindi cha kwanza na jingine wakalifunga kipindi cha pili.
Katika mchezo huo mchezaji Jeane Baleke alifunga ‘hat trick’ yake ya kwanza katika michuano hiyo ambayo bingwa ataiwakilisha nchi katika michuano ya Shirikisho barani Afrika msimu ujao.
Mabao mengine yalifungwa na Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho na bao la kufutia machozi lilifungwa na Raphael Loth.
Baada ya ushindi huo Simba itacheza katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam FC.