NA MWANDISHI WETU, GEITA
MWANAMME mmoja mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu mkoani hapa ( jina halijafahamika) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuunguza binti yake kwa moto mikono yote miwili.
Binti huyo Elizabeth Mathias mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ziwani Mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu Kata ya Nyarugusu aliunguzwa mikono yote miwili kwa kulowekwa kwenye maji ya moto na Baba yake mzazi baada ya kumkuta akiwa na shi.5000 ambazo alishindwa kueleza alikozitoa.
RPC wa Geita, Safia Jongo amekiri kumkamata Mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo huku akisema binti huyo amekuwa akilelewa na mama yake wa kambo ambaye pia alishiriki katika kutekeleza tukio hilo.
Kamanda Sofia amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutoa rai kwa Wananchi kuacha tibia za kuwaadhibu Watoto kikatili na kusema atakayekaidi atachukuliwa sheria.