NA WILLIAM KAPAWAGA, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Kikosi cha KMC, Thiery Hitimana, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania amesema kwamba kwa sasa wanapitia katika kipindi kigumu kutokana na matokeo ambayo wanapata kiwanjani.
Akizungumza na Demokrasia Kocha Mkuu wa timu hiyo Thiery Hitimana, amesema kutokana na kupoteza mechezo mingi ugenini ndio kumeifanya kufikia hatua hiyo.
Amesema wamepoteza michezo mingi ugenini kumewafanya wachezaji kushindwa kwa kujiamini.
Hitimana amesema timu yake ina kikosi bora miongoni mwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara lakini kwa sasa bahati haiku upande wao kutokana na kushishwa kufanya vizuri licha ya kuwa imara.
Amesema yeye kama sehemu ya benchi la ufundi amejitahidi kupambana ili kufanya vizuri lakini kutokana na kila timu kujipanga ndio maana hali hiyo imetokea ingawa ana amini watafanya vema katika michezo ambayo imeasalia ikiwamo wa leo.
Kocha huyo ambaye ameifanya timu hiyo kuhakikisha inacheza soka la kuvutia amesema kuwa atahakikisha kikosi hicho kinabaki Ligi Kuu msimu ujao.
“Nawaomba mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wanaendelea kuipa sapoti kubwa timu yao kwani atahakikisha timu hiyo haishuki daraja wala kucheza hatua ya mtoano kutokana na kikosi bora nilichonacho” amesema Hitimana.
Hata hiyo Kocha amewataka wachezaji kuhakikisha wanajituma kuhakikisha mechi zilizobaki wanapata matokeo yatakayoifanya timu hiyo iwe sehemu salama.