NA MWANDISHI WETU, SIMANJIRO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amemaliza ziara yake wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambapo pamoja na kukagua uhai wa Chama sanjari na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Katibu Mkuu Chongolo kwa mara ya kwanza katika historia ya CCM Wilaya ya Simanjiro aliitikia wito wa kulala kwenye shina namba 35, Tawi la Njiro Kata ya Orkesumeti.
Katibu Mkuu ambaye ameongozana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Ussi (Gavu).
Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amepata wasaa wa kuzungumza wasaa wa kuzungumza na Wenyeviti wa mashina yote ya kata ya Orkesumeti na kujumuika nao pamoja kwa chakula cha jioni.