NA JANETH JOVIN,DAR ES SALAAM
RAIS wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Akinumwi Adesina amesema kuwa Benki ya Dunia (WB) na AfDB wanalenga kutoa Dola za Marekani Bilioni 40 kama kianzio cha kuhakiksha wanafanikisha mpango wa kupeleka nishati ya umeme kwa wananchi barani Afrika.
Dk. Adesina ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika (Mission 300) unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Amesema patikanaji wa umeme ni jambo la muhimu katika bara la Afrika na ukosefu wa nishati hiyo unadhohofisha uchumi wa nchi moja moja.
“Asilimia kubwa ya waafrika kwa sasa hawana umeme na ndio maana tumeleta agenda hiyo ya Mission 300 ili kuhakikisha watu wanafikiwa na huduma hii ili kukuza uchumi wa nchi za Afrika,” amesema
Hata hivyo amesema hawataweza kufanikiwa jambo hilo kama hawataweza kufanyakazi pamoja na sekta binafsi na ndio maana wamefika katika mkutano huo kukubaliana ni kwa namna gani watatekeleza jambo hilo la kuwafikishia umeme watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira.