NA JANETH JOVIN,DAR RS SALAAM
ALIYEWAHI kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango, amethibitisha taarifa za kifo hicho cha Lowassa kilichotokea leo saa Nane mchana katika taasisi hiyo.
Kufuatia kifo hicho Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo.