NA MWANDISHI MAALUMU, JAKARTA,INDONESIA
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia lililofanyika leo Januari 25, 2024 katika jiji la Jakarta.
Kongamano hilo ni sehemu ya Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ilioanza Januari 24 , 2024 yenye lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi na hasa kuhamasisha biashara na Uwekezaji kwa pande zote mbili.
Taasisi mbalimbali za Sekta Binafsi na Umma pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wenzao wa Indonesia kubadilishana fursa baina yao.
Katika Kongamano hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyabiashara wa Indonesia na Tanzania mazingira mazuri yatakayoendelea kukuza biashara baina ya nchi hizi