NA MWANDISHI WETU,MPANDA,KATAVI
POLISI kata na watendaji wa kata zilizopo wilayani Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuratibu na kufanya doria za kutosha kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kudumisha amani, utulivu na usalama uliyopo Kwenye kata zao.
Wito huo umetolewa Leo Jumatano Julai 22, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani katika kikao kazi kilicho wakutanisha Polisi Kata na watendaji wa kata zote zilizopo Wilayani Mpanda kilichofanyika Ukumbi wa Polisi Kantini Manispaa ya Mpanda ambapo amewataka Polisi kata na watendaji kata kuhainisha maeneo korofi Kwenye kata zao na kuweka mikakati ya pamoja katika kufanya doria za kutosha kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutoa elimu kwa vikundi hivyo juu ya namna bora ya ufanyaji doria ikiwemo mbinu matumizi ya nguvu za kadri na ukamataji salama bila kuleta madhara kwa wakamataji wa watuhumiwa wa uhalifu na kuwafikisha vituo .
Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Katavi Mrakibu wa Polisi (SP) John Mwaipungu amewataka watendaji kata na Polisi kata hao kuendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi ikiwemo namna bora ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na kudhibiti wizi kwa njia ya mitandao kwa kujenga tabia ya kupiga simu kabla ya kutuma pesa ili kuhakiki endapo namba wanazozitumia pesa wanazitambua.
Aidha Mtendaji kata ya Ibindi, Moses Mihayo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kudumisha amani na utilivu inayoonekana katika maeneo yao pamoja na kuzidi kuwa karibu na wananchi kupitia Polisi kata na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea kufanya doria na misako ya mara kwa mara ili kutokomeza kabisa matukio ya kihalifu na wahalifu Kwenye makazi yao.

