NA MWANDISHI WETU,DODOMA
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume,Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Jumanne Aprili 14, 2026 amekutana na kuzungumza na jumbe maalum Jumuiya ya Madola (Commonwealth) Rais wa zamani wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera ambaye alitembelea ofisi za Tume Njedengwa jijini Dodoma.
Ziara hiyo maalum ya Mjumbe huyo wa Jumuiya ya Madola ililenga kuangalia namna Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ulivyofanyika.
(PICHA NA INEC).









