NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Halotel imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake nchini, baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya intaneti ya (5G) yenye kasi na ubora wa hali ya juu.
Uzinduzi wa huduma hiyo una lengo la kuwapatia wateja uzoefu mpya wa matumizi ya intaneti, ikiwemo kupakua na kupakia taarifa kwa kasi kubwa, mawasiliano ya video bila kukatika, pamoja na kuwezesha matumizi ya teknolojia za kisasa katika biashara, elimu na burudani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Halotel, Roxana Kadio amesema kampuni hiyo imekuwa ikitambua mahitaji ya wateja katika matumizi ya intaneti ya uhakika na yenye kasi, jambo lililoifanya kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya teknolojia ya 5G.
Kadio amesema huduma hiyo inalenga kuwafikia Watanzania wote waliopo mijini na vijijini, akibainisha kuwa kampuni hiyo inaamini asilimia kubwa ya wananchi wanatumia huduma ya intaneti kila siku. Kutokana na hali hiyo, Halotel imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuanzisha teknolojia ya intaneti ya kasi ya 5G.
“Halotel imejizatiti kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora, za uhakika na zinazoendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani hivyo huduma ya 5G ni sehemu ya mkakati wetu wa muda mrefu wa kuboresha mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kidijitali nchini.
“Mtumiaji yeyote mwenye simu janja anaweza kufurahia huduma ya 5G kutoka Halotel. Huduma hii imeenea nchini kote, na wateja wakitembelea maduka yetu wataweza kupata ‘router’ maalum itakayowawezesha kutumia intaneti ya 5G. Tumejipanga vizuri katika huduma hii kwa kuanzisha vifurushi (bando) mbalimbali ambavyo tunaamini vitawafurahisha wateja wetu katika matumizi yao ya kila siku ya intaneti,” amesema Kadio
Aidha, amesema kuwa kampuni hiyo ina furaha kumtangaza msanii Idriss Sultan kuwa balozi wao rasmi, ambaye atakuwa mstari wa mbele kutangaza na kubeba bendera ya huduma zote zinazotolewa na Halotel, ikiwemo huduma hiyo ya 5G inayopatikana kote nchini.
Karina hatua nyingine,Msanii na mjasiriamali maarufu nchini, Idris Sultan amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa zilizopo kwenye intaneti kama nyenzo muhimu ya kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi, akisisitiza kuwa dunia ya sasa inahitaji ubunifu na matumizi sahihi ya teknolojia.
“Tayari sasa hivi kila kitu inachokiona kipo mtandaoni hivyo Intaneti siyo kwa ajili ya burudani pekee. Ni soko kubwa sana. Ukiitumia vizuri, unaweza kupata wateja kutoka sehemu yeyote bila hata kuwa na duka la kawaida, hivyo 5G ya Halotel ina kasi ya kutosha itakayokuwezesha kufanyashughuli mbalimbali mtandaoi,” amesema Sultan
Amewahimiza vijana kuwekeza muda wao kujifunza ujuzi mbalimbali mtandaoni ikiwemo masoko ya kidijitali, uundaji wa maudhui, huduma za mtandaoni pamoja na mbinu za kuwafikia wateja kwa gharama ndogo lakini kwa ufanisi mkubwa.
Alipoulizwa kwanini amekuwa akipata dili mbalimbali, msanii huyo kila msanii ananamna anavyofanya kazi hivyo wateja uangalia mtu anayeweza kufanyanaye kazi kwa namna anavyojiweka katika shughuli zake.





