BAADHI ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya VODACOM PLC wakiwa na nyuso za furaha huku wakiwa wameshikilia Tuzo ya Mshindi wa Kwanza katika Sekta ya Mawasiliano kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimaitaifa ya 48 yaliyofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam kuanzia Juni 28,2024 hadi Julai 14 ,2024.Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa VODACOM na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika kufunga Maonesho hayo Julai 13,2024.