FLORAH AMON,DAR ES SALAAM
BENKI ya QUITY Tanzania imeonesha dhamira yake ya kuendelea kuleta mageuzi katika sekta ya huduma za kifedha nchini kwa kuwekeza zaidi katika teknolojia za kidijitali, kupanua mtandao wa matawi na mawakala, pamoja na kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ambapo hatua hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo wa kukuza ujumuishaji wa kifedha na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 8,2025 jijini Dar es Salaam, ktoba 2025, katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Isabella Maganga, amesema benki hiyo inaendelea kutumia ubunifu na teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinafika kwa urahisi na usalama kwa watu wa kada zote, hususan walioko maeneo ya mbali.

“Kaulimbiu yetu ya mwaka huu, ‘Mission is Possible’, inaashiria dhamira yetu ya kuwasaidia wateja kufikia malengo yao ya kifedha tumetengeneza bidhaa nafuu na jumuishi ambazo zinawagusa zaidi watu wa kipato cha chini,” amesema Maganga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Equity Bank Tanzania, Bwana Prosper Nambaya, amebainisha kuwa benki hiyo imekuwa ikipanua huduma zake kupitia ongezeko la matawi, mawakala, na pia kwa njia za kidijitali kama benki mtandao na programu za simu.
“Hadi sasa tuna zaidi ya mawakala 3,000 nchini kote, na tunalenga kuwa na matawi 55 kufikia mwaka 2030. Kupitia ushirikiano wetu na Umoja Switch, wateja wetu wanaweza sasa kupata huduma kupitia zaidi ya ATM 1,000 nchini,” ameeleza Nambaya.

Kwa baadhi ya wateja wa benki hiyo wameezea namna ambavyo huduma za Equity Benk zimewasaidia kukuza biashara na kuongeza ufanisi katika shughuli zao.
Uinde Muro, Mkurugenzi wa Imperium OpEx, amesema huduma za benki hiyo zimekuwa rafiki kwa wateja na zimezingatia mahitaji halisi ya wajasiriamali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya GSM,Benson Maenya, ameeleza kuwa ushirikiano wake na Equity Bank umekuwa na mchango mkubwa katika upanuzi wa biashara zake ndani ya Afrika Mashariki, hasa kutokana na mtandao mpana wa benki hiyo na ubora wa huduma zake.
Kwa ujumla, mikakati ya Equity Bank Tanzania inaonyesha namna taasisi hiyo inavyojikita katika kuondoa vikwazo vya kifedha, kukuza ujumuishaji wa kifedha, na kuboresha maisha ya wananchi kupitia huduma bora, nafuu na zinazopatikana kirahisi.

