NA MWANDISHI WETU,MBEYA

WIZARA ya Kilimo imezindua Kampeni ya kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima iliyopewa jina la ‘ Mali Shamba ,Silaha Mbolea’ jijini Mbeya
Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo Oktoba 7,3025 Naibu Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dk.Stephen Nindi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan inatambua mchango mkubwa wa mbolea katika kukuza kilimo na uchumi wa Taifa

Dk Nindi aliongeza kuwa,kutokana na utambuzi huo ndiyo maana Serikali imeendelea kutoa ruzuku kwenye mbolea zote, ili kuhakikisha wakulima wananunua kwa bei nafuu na wanatumia ipasavyo katika mashamba yao.

Naibu Katibu Mkuu Dk.Nindi amesema ruzuku inatolewa kupitia Mfumo wa Pembejeo za Ruzuku, hivyo wakulima wote wanasisitizwa kujisajili katika mfumo huu ili waweze kunufaika na bei ya ruzukuna kupata pembejeo kwa wakati.

Serikali inatoa “Silaha Mbolea” kwa gharama nafuu kupitia ruzuku, hivyo ametoa wito kwa wakulima wote kuhakikisha wanajisajili ili wapate fursa muhimu ya kuboresha uzalishaji wao.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Samuel Mshote, amesema moja kati ya majukumu yake ni kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa mbolea kwa ajili ya wakulima wa nchi hii
“Haya yote yanafanyika ili kuhakikisha wanafanya uwekezaji kwa kutumia rasilimali za ndani au madini ya ndani ili kuweza kuzalisha mbolea ambazo zitatumika na wakulima ambazo zinaendana na afya ya udongo na aina ya zao ambao wakulima wanalima” amesisitiza Mkurugenzi huyo wa TFC

