NA MWANDISHI WETU,SONGWE
MKUU wa Wilaya ya Songwe, Mheshimiwa Fadhili Nkurlu, amezindua vifaa vya kutambua na kudhibiti moto katika Shule ya Sekondari Kanga, ikiwa ni juhudi za kuimarisha usalama shuleni.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi, walimu na wanafunzi, DC Nkurlu alisema hatua hiyo inalenga kupunguza athari za moto kwenye taasisi za elimu, hasa shule za bweni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, CPA Cecilia Kavishe, aliahidi kuendelea kusambaza vifaa hivyo kwenye shule nyingine za bweni wilayani humo

Kwa upande wake, Mkuu wa shule, Ester Ole Kimani, alisema walimu na wanafunzi wamepewa mafunzo ya kutumia vifaa hivyo na mbinu za kujikinga dhidi ya moto. Wanafunzi walifanya maonesho ya vitendo kuthibitisha uelewa wao.

Jamii imepongeza hatua hiyo, ikihimiza usambazaji wa teknolojia hiyo kwenye shule zote nchini.

