NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
JUKWAA la Kidijitali la PIKU linaloendesha minada ya kipekee mtandaoni, limetangaza na kukabidhi zawadi kabambe kwa watu watatu walioibuka washindi kwa kujipatia bidhaa za kisasa na za thamani kupitia mnada huo.
Mshindi wa kwanza katika mnada huo ni Jenipher Ayoub ambaye amejinyakulia zawadi kubwa zikiwemo friji, jiko janja lenye sahani nne (tatu za gesi na moja ya umeme), mashine ya kufulia, vifaa vya jikoni pamoja na kifaa cha kuchakata vyakula (food processor).
Mshindi wa pili, Michel Ezekiel, amepokea simu, bando la mwaka mzima kutoka Airtel na spika za bluetooth, huku mshindi wa tatu, Niyovita Shayo akijishindia seti ya vipodozi na saa ya kike ya mkononi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, aliwapongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kujiunga katika minada yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kubadili maisha.
Amesema kuwa bado kuna zawadi mbalimbali ikiwemo gari, televisheni, pikipiki, dhahabu, simu janja na nyinginezo huku akifafanua kuwa jukwaa la kidijitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee na yenye ushindani wa hali ya juu.
Mbunda amesema kuwa mipango yao mikubwa ni kupanua wigo wa mnada wao ikiwa pamoja na kuwezesha washindi kupata zawadi ya kushuhudia mbashara mchezo wa Yanga na Simba na michezo mengine ya ligi kuu mbalimbali duniani.
“Baada ya siku 28, mshindi atakayetoa dau dogo na la kipekee atajipatia pikipiki mpya aina ya TVS yenye helmeti, kiakisi mwanga, kadi ya mafuta ya miezi sita na bima, pamoja na gari aina ya Raum,” amesema Mbunda.
Mbunda ameongeza kuwa lengo la PIKU ni kupanua wigo wa huduma na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushindania bidhaa zenye thamani kubwa.
Aidha, ameeleza utaratibu wa ununuzi wa tiketi ambapo tiketi 10 zinapatikana kwa Sh.1,000, tiketi 50 kwa Sh.5,000, tiketi 100 kwa Sh.10,000 na tiketi 1,000 kwa Sh.100,000, akibainisha kuwa kadri tiketi zinavyoongezeka ndivyo nafasi ya ushindi inavyokuwa kubwa zaidi.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Vivian Mboya, amesema mnada huo umefanyika kwa kufuata kanuni na taratibu rasmi, na washindi wote wamepokea zawadi zao kihalali.
“Nawaomba Watanzania kushiriki katika mnada wa Piku na kujishindia zawadi mbalimbali, kampuni inaendesha droo yao kwa uwazi na zawadi zinawafikia washind pia zawadi zao wanatoa kwa kufuata taratibu, sheria na vigezo vilivyowekwa,” amesema.
Akieleza furaha yake, mshindi wa kwanza Ayoub, ambaye alitoa dau la Sh.36,000 pekee na kushinda bidhaa zenye thamani ya Sh. milioni 4 kutoka kampuni ya LG, ameipongeza PIKU Afrika kwa kufanya minada ya kweli mtandaoni.
“Niliona tangazo Instagram, nikaamua kujaribu, na hatimaye nikashinda zawadi ambazo sikutegemea. Nawashukuru sana PIKU,” amesema kwa furaha.
Naye Shayo amesema mnada wa piku aliuona kupitia ndugu yake na alipocheza kwa Mara ya kwanza aliyoenda kwani wa uwazi hivyo anaishukuru Kampuni ya Piku kwa kubuni na kuleta kitu Kama hicho ili vijana wako Tanzania waweze kujishindia bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake Ezekiel ambaye pia ni mshindi wa Piku amesema mnada huo waliuona katika mitandao ya kijamii na anashukuru kwa kuweza kushinda zawadi hizo na kwamba atakuwa balozi mzuri kwa watu wengine katika kuutangaza mnada huo.