NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) katika kutekeleza majukumu yake ya kuhamasisha Umma matumizi ya chapa ya bidhaa na huduma zinazozalishwa Tanzania, ‘Made in Tanzania’ imeandaa banda maalum kwenye mkutano wa nchi za SADC.
Banda hilo linalokutanisha wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali.
Banda la Made in Tanzania limekuwa kivutio kwa watu wengi kwani kuna kampuni inayofahamika kwa jina la ‘The Tanzanite Experience’imeweza kuleta na kuweka bidhaa za urembo wa madini aina ya Tanzanite, yanayozalishwa nchini Tanzania.
Mkakati wa TanTrade ni kuhakikisha bidhaa za wazawa zinatangazwa zaidi kwenye masoko ya Kimataifa na kutambulika kirahisi duniani kote.
Banda la Made in Tanzania lipo katika ukumbi wa mikutano wa JINCC, Jijini Dar es Salaam.