NA MWANDISHI WETU
WAKALA WA VIPIMO( WMA) wamezindua rasmi Jarida lao la mtandaoni liitwlo Mbiu ya Vipimo jana Oktoba 3, 2024 .
Jarida hilo limwzinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dk Hashil Abdallah.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa WMA ,Veronica Simba,Mbiu ya Vipimo itakuwa inatoka kila robo ya mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu.
Simba ameeleza kuwa, Toleo hilo la kwanza, linajumuisha robo ya kwanza ya Mwaka huu wa Fedha (Julai, Agosti na Septemba)
“Nawakaribisha sasa muipokee MBIU YA VIPIMO Toleo la Kwanza, muisome na muhimu zaidi mtusaidie kuisambaza kwa wadau wengine kwa wingi.” amesema Simba