NA PETER HAULE,WF,DAR ES SALAAM
WIZARA ya Fedha imeibuka Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Aidha, Taasisi yake ya Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi (PPRA) imeshika nafasi ya Kwanza kwa upande wa Mamlaka za Udhibiti nchini, huku Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA), ikishika nafasi ya Pili katika kundi la Taasisi za Serikali