NA ASHRACK MIRAJI,SAME
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akitoa heshima ya mwisho kwa aliyekua Katibu tawala wa mkoa huo Dk.Tixon Nzunda, nyumbani kwake Manispaa ya Moshi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salam na baadaye mkoani Songwe kutakapo fanyika shughuli za maziko.
“Wananchi wa Wilaya ya Same tutaendelea kukumbuka busara na hekima zako kwenye uongozi, ni ngumu kuamini lakini kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu kuwa mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi (Ayubu 14:1-2) hatuna namna nyingine zaidi ya kukuombea kwenye maisha mengine huko mbele za mungu”.
Nzunda alifariki dunia yeye na dereva wake Alphonce Edson kwenye ajali ya barabarani Juni 18, 2024 wilayani Hai alipokua kwenye majukumu ya kikazi.