NA JANETH JOVIN, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea inaenda kuleta mafanikio makubwa nchini katika nyanja ya Kiuchumi,Kiteknolojia kwa kufanya utafiti wa rasilimali za baharini,Ijiolojia za Madini,Masuala ya Gesi,Kukuza Bunifu na kuongeza uwekezaji katika uchumi wa bluu.
Akizungumza leo Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa habari, Yunus amesema Rais Samia alifanya ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Yeol pamoja na kuhudhuria mkutano wa ushirikiano baina ya Korea na Afrika(Korea, Afrika Summit).
Amesema ziara hiyo ya Rais Samia itaweza kufanya Tanzania kuongezewa uwezo katika teknolojia ya ijiolojia ya kufanya utafiti zaidi ya madini ya kimkakati pamoja na uongezaji thamani ya madini hayo kwa kupata utaalam madhubutu kutoka korea.
Yunus amesema pia Tanzania itaweza kupata maabara ya kisasa na kufanikiwa kuingia katika Mpango wa ushirikiano wa miaka mitano ambapo umewezesha Tanzania kupokea mkopo nafuu kutoka korea wa kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024 hadi 2028 kwaajili ya miradi ya miundombinu maendeleo.
”Fedha hizi zinatolewa katika Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea na Mkopo huo utaanza kulipwa baada ya miaka 25 na utalipwa kwa miaka 40 kwa riba ya asilimia 0.01 kwa muda wote wa malipo,”amesema na kuongeza
”Mafanikio mengine ni kuingia katika mkataba mwingine uliosaini ambao ni wa shirikiano wa dolla za kimarekani milioni 163.6 kwaajili ya kuimarisha huduma za afya,teknolojia ya kisasa katika matibabu na kujenga uwezo wataalamu wa tiba fedha hizi zitatumika kujenga hospitali ya kisasa ya binguni,visiwani Zanzibar,”amesema.
Amesema fedha hizo nazi ni za mkopo ambao ni nafuu na utakaolipwa kipindi cha miaka 40 kuanzia mwaka wa 26 na riba hiyo hiyo ya asilimia 0.01.
Mbali na mikopo hiyo, Yunus amesema katika mazungumzo waliyofanya Marais hao pia Rais Samia alipendekeza ushirikiano na Korea katika sekta nyingine zitakazoleta manufaa zaidi ni pamoja na Suala la gesi ambapo mazungumzo yameanza na TPDC, mafunzo ya anga, sekta ya ubunifu na filamu, suala la madini kimakakati.
Mbali na mikataba kusainiwa, amesema pia kulikuwa na mkutano wa Afrika na Korea ambapo Rais Samia alihudhulia Mkutano huo na Viongozi mbalimbali wa nchi wa Juu wa nchi za Afrika ambapo ambapo Rais Samia ,alisisitiza ushirikiano wa kiuchumi na teknolojia kwa nchi za Afrika na kuona namna ya nchi ya Korea ilivyokuwa mbali.
Amesema kwa kuimarisha ushirikiano huo kuna uwezekano na faida kubwa kwa nchi za bara la afrika kukua kibiashara na uwekezaji katika sekta binafsi.
Aidha amesema katika ziara hiyo Rais Samia alikutana na Watendaji Wakuu wa Kampuni kubwa nchini Korea ambayo kati yao yapo yanayotarajia kuja kuwekeza Tanzania na mengine tayari yamewekeza.
Akiongelea suala la utunukiwaji wa Udaktari Rais Samia, Yunus amesema Dk. Samia alitunukuwa udaktari wa Falsafa wa heshima katika sekta ya anga na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga,ambapo Mkuu wa Chuo hicho alitaja sababu za kumtunuku Rais Samia Udaktari huo.
Amesema miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na Dkt. Samia kuwa kinara wa Mabadiliko ya Tabianchi,Nishati safi ya kupikia barani Afrika,Maendeleo ya Miundombinu kwenye viwanja vya Ndege ikiwemo Doodoma,Kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuongeza idadi ya ndege.
Pia alitaja sababu nyingine ni pamoja na Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania kuongeza safari zake za kitaifa na Kimataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nchini Tanzania kufika maeneo 24,Kwa bara ya Afrika kufanya safari nane za miji na tatu za kimataifa.
Yunus aliongeza pia waliangalia namna ya rubani waliosajiliwa hadi sasa ni 604 sawa na ongezeko la asilimia 21 na wahandisi 76 sawa na ongezeko la asilimia 181 mpaka mwisho wa mwaka 2023 vitu ambavyo vilipelekewa kupata udaktari huo.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,January Makamba amesema ziara hiyo ya Rais Samia ni moja ya ushirikiano wa kimataifa wa kimaendeleo baina ya nchi ya Tanzania na Korea.
”Viongozi wanaposafiri na Tanzania kuingia katika mazungumzo na nchi nyingine ni katika kutekeleza sera ya nchi ya mambo ya nje ambayo inaelekeza hivyo,”amesema.
Amesema dunia ya sasa ni ya ushindani na ushirikiano,hivyo nchi zimekuwa zinashindana kwa kuvutia mitaji,kutafuta masoko,kupata maarifa ya maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto za kidunia zinahitaji majadiliano ili kuzitatua ikiwemo masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
”Maarifa za viongozi lazima yaweze mambo yote mawili ushirikiano na ushindani na katika kuyapata yote lazima kutafuta washirika wa kushirikiana nao na rafiki wa kweli wa kuweza kuhimili ushindani na kupata maarifa ya kutimiza maendeleo ya nchi,”amesema.
Amesema dunia ya sasa ilipofikia sio ya kukaa ndani ya mipaka yako bila kutoka nje ya mipaka na kuzungumza na dunia ambayo ina uwezo wa kusaidia kutimiza maendeleo ya ndani
.”Kwenye dunia ukijifunguia na kusema hutaki kuzungumza na mtu hata maendeleo ya ndani hayawezi kutimi,”amesema.
Amesema dunia ya sasa ni ya ushindani na ushirikiano,hivyo nchi zimekuwa zinashindana kwa kuvutia mitaji,kutafuta masoko,kupata maarifa ya maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto za kidunia zinahitaji majadiliano ili kuzitatua ikiwemo masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
”Maarifa za viongozi lazima yaweze mambo yote mawili ushirikiano na ushindani na katika kuyapata yote lazima kutafuta washirika wa kushirikiana nao na rafiki wa kweli wa kuweza kuhimiri ushindani na kupata maarifa ya kutimiza maendeleo ya nchi,”amesema.
Amesema dunia ya sasa ilipofikia sio ya kukaa ndani ya mipaka yako bila kutoka nje ya mipaka na kuzungumza na dunia ambayo inauwezo wa kusaidia kutimiza maendeleo ya ndani .
”Kwenye dunia ukijifungia na kusema hutaki kuzungumza na mtu hata maendeleo ya ndani hayawezi kutimia,”amesema.