NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha inafanya maboresho kwenye mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu hususani pampu za kusukuma maji ili kuwezesha huduma ya maji iweze kupatikana kwa ufasaha na kwa wananchi wote.
Waziri Aweso ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea na kukagua hali ya uzalishaji na upatikanaji huduma ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kujiridhisha juu ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwenye chanzo cha maji Mto Ruvu Machi 7,2024
Ameongeza kwa kusema ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa maji kutoka Mto Ruvu na kuwa mitambo ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini maji yapo ya kutosha, hivyo kazi kubwa inayohitaji kufanyika ni maboresho ya pampu za kusukuma maji kwenye ili huduma iweze kupatikana.