NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa BODI ya Wakala wa Nishati Vijijini(REA)Sophia Mgonja ametoa wito kwa wanawake kutumia nishati safi.
Mgonja aliyasema hayo Machi 7,2024 ikiwa ni sehemu ya salamu zake za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa leo Machi 8,2024 Duniani kote.
Mgonja amesema wanawake wanatakiwa kutumia Nishati safi na kuachana na kuni ili kuepuka magonjwa.
Amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa kuongoza njia katika matumizi ya nishati safi.
“Wanawake tujitahidi kutumia nishati safi kwasababu serikali inaongoza njia hivyo basi na sisi tunatakiwa tufuate jinsi serikali inavyotaka ili kupunguza magonjwa yatokanayo na matumizi ya kuni
“Hizi ni salamu zangu katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu” alihitimisha Mjumbe huyo wa Bodi REA