Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Februari 22, 2024Balozi Shaibu Musa – Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba Katibu Mkuu akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) wakizungumza wakati wa mkutano wa Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Februari 22,2024.Balozi Shaibu Musa – Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri wakati mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Wahariri na Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi Ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, leo februari 22, 2024.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, leo Februari 22, 2024.
NA JANETH JOVIN,DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa wafanyabiashara wa sukari 84 wamekamatwa na hivi karibuni watafikishwa mahakamani kutokana na kufanya ujanja ujanja katika suala la uuzaji wa sukari hapa nchini.
Bashe amebainisha hayo leo Februari 22,2024 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari ambapo amesema operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara itaendelea mpaka pale bei itakaporudi kuwa kawaida.
Amesema wafanyabiashara wana machaguo mawili moja waache kuuza sukari serikali itatafuta njia nyingine na wenye viwanda nao wanamachagua mawili wafuate utaratibu wa serikali na kama hawawezi waache hio kazi.
“Pia tumewapelekea walaka wa kubadilisha mfumo wa usambazaji, haiwezekani mfano Kagera Sugar ana msambazaji mmoja yupo Mwanza anahudumia mikoa 11, serikali haiwezi kuruhusu hili,” amesema Bashe na kuongeza
“Tuna changamoto kubwa ya wafanyabishara hasa wa rejareja kufanya uhuni hivyo hadi sasa tupo katika hatua za mwisho kuwapeleka mahakamani, nini kinatokea sukari inaingia anauziwa kati ya 2500 hadi 2800 na importer, akinunua yeye anakwenda kuuza 4000 hadi 4500 wakati tayari sisi tumeshatoa bei elekezi
Amesema tatizo la bei sasa hivi ni la mpito, wanaamini mpaka kufika katikati ya mwezi Machi watakuwa wameingiza nchini tani 60,000 za sukari, hivyo hadi kufikia mfungo wa mwezi wa Ramadhani hali itakuwa nzuri.
Waziri Bashe amesema wataendelea kuigiza sukari hadi pale watakapoona hali imetengamaa