NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkuu wa masoko na mauzo Barnes Hampel wa timu ya Chelsea ya England na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo Februari Mosi, 2024.
Katika mazungumzo yao wamezungumzia kuhusu kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii na kuanzishwa kwa Academy za mpira wa miguu nchini.