KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Balozi Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wakiwa kwenye mazungumzo mazito kuhusu masuala mbalimbali, baada ya Waziri huyo kumtembelea Katibu Mkuu wa CCM Nchimbi ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma, leo Alhamisi, Februari 1, 2024.