NA TERESIA MHAGAMA,DAR ES SALAAM
NAIBUWaziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko leo Januari 22,2024
ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China,
Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.
Akiwa nchini, Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu
Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim Majaliwa.
Pia atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), Reli ya TAZARA na eneo la makaburi ya Wataalamu wa
kichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA pamoja na
Makumbusho ya Taifa.

akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Chen
Mingjian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
jijini Dar es Salaam kabla ya kuwasili kwa Naibu Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Watu wa China,Liu Guozhong.

pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto
Biteko wakisalimia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini
Dar es Salaam.

akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China,
Liu Guozhong ambaye amewasili nchini kwa ziara ya siku tatu.

akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya Siku Tatu. Katika uwanja huo amepokewa
na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko.