NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UBALOZI wa Marekani nchini Tanzania unatarajia kufanya maadhimisho ya Kiswahili katika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2023.
Mgeni maalumu katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Consolata Mushi.
Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo, maadhimisho hayo yatayayofanyika kwenye ofisi za ubalozi yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 10:30 jioni.