NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KLABU ya Soka ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) imetangaza kumalizana na kiungo wake Feisal Salum kwa kumuuza kwenda klabu ya Azam
Idara ya Mawasiliano ya klabu hiyo imetoa taarifa mapema leo Juni 8, 2023 ikisema imepokea ofa kutoka klabu ya Azam ya kumuhitaji mchezaji wake.
Taarifa hilo imesema Feisal ameuzwa kwanta Azam kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
Yanga wamesema kilichobaki ni makubaliano binafsi kati ya Azam na Feisal.
Klabu hiyo iliingia kwenye mgogoro na mchezaji huyo baada ya Feisal kulazimisha kuhamia klabu ya Azam kwa kuununua mkataba wake juhudi ambazo ziligonga mwamba na kumfanya akae nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita.