NA MWANDISHI WETU
KLABU ya Soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imempa mkataba mpya mlinzi wao kinda, Ibrahim Abdallah (Bacca).
Kizungumza jijini Dar es Salaam Leo Jumatatu, Mei 5, Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said amesema wameshamalizana na mlinzi huyo kwa kumpatia mkataba mnono ili asalie kwenye klabu hiyo.
Siwezi kuusema mkataba wenyewe ni wa kiwango gani, lakini ni mkataba mnono ambao unaendana na kiwango chake kikubwa alichokionesha kwenye michuano ya msimu huu kwa klabu na timu ya taifa.
Sio busara niweke wazi kila kitu kwasababu mkataba ni siri ya mwajiri na mwajiriwa. Itoshe tu kusema tumeshamalizana nae” alisema Hersi
Bacca ni mmoja ya Wachezaji walioonesha kiwango kikubwa cha soka kilichopelekea kuipa Yanga ubingwa wa Ligi na kuifikisha finali ya Kombe la Shirikisho Afrika