NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
LIFTI iliyopo katika jengo la ghorofa la Millenium ‘Millenium Tower’ Makumbusho, jijini hapa, imeporomoka na kujeruhi watu saba huku chanzo kikitajwa kushindwa kuhimili uzito mkubwa kinyume na uzito unaotakiwa.
Akizungumza juu ya ajali hiyo Kamishna Msaidizi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni (ACF) Christina Sunga amesema: hayupo eneo la tukio, ila anafanya mawasiliano na waliopo eneo la tukio hilo.
Hata hivyo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi hilo Patrick Afande ameeleza kuwa chanzo cha lifti hiyo kuporomoka ni kuzidisha idadi ya watu tofauti na uwezo wake ambapo wakati tukio hilo linatokea ilibeba zaidi ya watu 10.
Lifti hiyo imeporomoka kutoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa matibabu.