NA MWANDISHI WETU, TANGA
WANANCHI wanaendelea kufurika katika Kambi Maalum ya Macho Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bomba Jijini Tanga kupata huduma ikiwa leo ni siku ya mwisho ya Kambi ya matibabu ya macho, kugawa miwani na huduma zingine za afya bure.
Akizungumza na Demokrasia Daktari Bingwa wa Macho Majala Majala alisema kuwa zaidi ya watu 300 wamefanyiwa upasuaji wa macho na kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje zaidi ya 5000.
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza kuchukua nafasi hii kutibiwa bure na kujua afya zao za macho.
“Nashukuru leo ni siku ya mwisho ya Kambi hii hapa Jijini Tanga namshukuru Mungu wagonjwa wameitikia wito vizuri kwani siku ya kwanza tu tumeandikisha wagonjwa zaidi ya1000 na bado wanaongezeka kujitokeza leo ikiwa ni siku ya mwisho alifafanua zaidi Dkt Majala.
Naye Amina Omari kutoka kijijini Tanganyika ameipongeza Kambi hiyo kwa kazi nzuri ya huduma ya macho japo walianza kwa kasi ndogo .
“Nashukuru sana nimehudumia vuziri nimepata miwani sasa hivi naondoka, naomba waje tena mara kwa mara” alisitiza Amina.
Kambi hiyo ya Macho ya siku tatu kuanzia Mei 19, 2023 imeratibiwa na Lions Club toka Dar ea Salaam.
Mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2019 Jijini Tanga.