NA MWANDISHI WETU, LUSHOTO
SERIKALI Wilayani Lushoto Mkoani Tanga imegawa jumla ya miche 227,905 ya zao la kahawa bure kwa wakulima lengo kuhamasisha kilimo hicho.
Miche hiyo imegawiwa kwa wakulima ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wakulima kulima zao hilo likiwa mojaapo la kimkakati la kibiashara wilayani hapa
Akizungumza kwenye hafla fupi ya ugawaji huo mwishoni mwa wiki mjini Lushoto Mkuu wa Wilaya hiyo Kalisti Lazaro amesema zao hilo la kahawa ni la tano kimkakati baada ya zao la chai, Parachichi, Ngano na Mkonge wilayani Lushoto.
Alisema mwaka jana Bodi ya Kahawa ilitoa miche zaidi ya 69,000 na wakaanzisha kitalu hadi sasa wana miche zaidi ya 300,000 na wataendelea kusambaza kwenye majimbo matatu ya Lushoto, Bumbuli na Mlalo wilayani hapa.
Amewataka wananchi wa Lushoto kuona umihumu wa kulima mazao ya kudumu la kahawa kwani soko lake kwa sasa lina bei nzuri.
Naye Mkulima wa wa zao hilo Siwema Rashid aliishukuru serikali kwa juhudi ya kuhamasisha na kufufua kilimo cha kahawa ambayo kutokana miaka ya nyuma bei kushuka sana sokoni.