NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
WAAJIRIWA wa Sekta Binafsi na Sekta Isiyo Rasmi hasa wajasiriamali wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kujiwekea akiba Kupata fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoratibiwa na mfuko huo.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri, ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Patrobas Katambi kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usalama mahala pa kazi, Mjini Morogoro yaliyoratibiwa na Wakala wa usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Akizungumza alipotembelea banda la NSSF kujionea namna mfuko huo unavotekeleza majukumu yake ya usalama na afya mahala pa kazi amesema ni vyema watanzania Wote wenye sifa za kujiunga na mfuko huo wajiunge.
Aidha Naibu waziri Katambi amepongeza jitihada za NSSF kwa kuboresha huduma kwa Kutoa huduma kimtandao hali inayowarahisishia wateja wake kupata taarifa wakati wowote.