NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Pindi Chana amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumsimamisha kazi Kaimu meneja wa uwanja huo, Said Mtumbuka na wafanyakazi wengine sita kutokana na kukatika kwa umeme katika uwanja huo katika mechi ya kombe la shirikisho Afrika kai ya Yanga na Rivers United kutokea Nigeria
Taarifa iliyotolewa jana Aprili 30 , 2023 waliosimamishwa ni aliyekuwa Mhandisi wa Umeme, Manyori Kapesa na aliyekuwa Ofisa Tawala wa Uwanja huo, Tuswege Nikupala.
Aidha, rungu hilo pia limewapitia wafanyakazi wengine wa uwanja huo akiwemo, Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano.
Taarifa hiyo pia imesema Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Said Yakubu amemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa uwanja huo kuanzia leo Jumatatu Mei 1, 2023.
Pia, Katibu Mkuu atawasiliana na wadau wote kuwa mechi zote zitakazochezwa uwanjani hapo zipangiwe jioni na sio usiku katika kipindi hiki ambacho maboresho ya mfumo wa umeme na taa unaendelea.
Kwa upande wao Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitia taarifa yake rasmi iliyotolewa na kurugenzi yao ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma imesema haihusiki na kukatika kwa umeme katika uwanja huo.
“Tanesco inawataarifu kuwa uwanja wa Taifa unahudumiwa na vyanzo viwili vya umeme, Tanesco na majenerata ya uwanja huo. Katika mechi ya leo (Yanga na Rivers United) uwanja ulikuwa unahudumiwa na majenereta,”.
Pia, wamesema baada ya majenereta kushindwa kufanya kazi katikati ya mchezo ndipo walitumia umeme wa Tanesco na mechi ikaendelea