LAGOS, NIGERIA
TIMu ya Yanga ya Dar es Salaam, Tanzania imetetema nchini Nigeria kwa kuifurisha Rivers United kwa magoli 2-0.
Yanga wakicheza kwa kujiamini walipata goli la kwanza kwenye dakika ya 73 ya mchezo, bao lililowekwa kambani na Mkongo Fiston Mayele
Mayele aliiandikia bao la pili timu yake baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mwamnyeto kwa faida ya ‘counter attack’
Bao hilo la pili kutoka kwa Mayele limemfanya awe mchezaji anayeongoza kwa magoli akiwa amezifumania nyavu mara tano huku anayemfuata akiwa na magoli matatu.
Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipenga cha mwisho, miamba hiyo ya Jangwani imeweka kwapani alama tatu na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga nusi fainali ya kombe hilo la shirikisho barani Afrika.
Mchezo wa pili wa robo fainali hiyo utafanyika Dar es Salaam, Jumamosi Aprili 29, 2023.