NAIROBI, KENYA
BONDIA Kareem Mandonga (Mtu kazi) amemshinda raia wa Uganda, Kenneth Lukyamuzi kwenye pambano la ndondi na kutwaa taji lake la kwanza kwenye historia ya mchezo huo.
Mandonga mwenye mashabiki wengi nchini Kenya, hususan jijini Nairobi, alikutana na mshindani wake huyo kwenye mchezo uliopigwa kwenye kiwanja cha Kasarani , pambano ambalo lilikuwa la mizunguko minane.
Akishangiliwa na mashabiki lukuki kama yupo kwenye ardhi ya nyumbani, Mandonga aliweza kukwepa ngumi kali za mpinzani wake aliyemzidi urefu lakini mwenye gumi za kushtukiza zilizojaa uzito.
Mabondia wote walifanikiwa kumaliza pambano lao la mizunguko minane wakiwa bado wana nguvu kabla ya kumpa Mandonga ushindi kwa alama nyingi zaidi ya mpinzani wake.