Usajili wa Lukaku wakosolewa Inter Milan
MILAN, ITALIA
WACHAMBUZI wa masuala ya michezo nchini Italia wamesema kwa katika usajili ambao ulifanywa na Inter wababe wa Serie A katika majira ya kiangazi wameboronga.
Jarida la La Gazzetta dello Sport nchini humo limesema kwamba usajili wa wachezaji,Romelu Lukaku haukustahili kwa kuwa wamekuwa ni miongoni mwa waliocheza vibaya na kutokuwa na msaada katika timu yao.
Inter ilimtegemea sana Lukaku kushinda taji lao la pili la Serie A ndani ya misimu mitatu, lakini fowadi huyo wa Ubelgiji amekuwa na majeraha akifunga mabao matano pekee katika mechi 19 alizocheza.
Pia inaelezwa huenda mchezaji huyo katika dirisha la usajili lijalo atazamiwa kutua katika kikosi cha Chelsea.
Nacho hatihati kubaki Santiago Bernabeu
MADRID, HISPANIA
BEKI mkongwe wa kikosi cha Real Madrid, Nacho Fernandez, huenda aongezewe mkataba mpya kutokana na kuonekana kupungua kiwango.
Mkataba wa mwanandinga huyo inaelezewa kwa sasa unakwenda ukingoni mwishoni mwa msimu huu na hakuna dalili ya kumuongezea.
Hivi karibuni akifanya mazungumzo na moja ya chombo cha habari nchini humo alikaririwa akisema kuwa kusalia katika klabu hiyo itategemea ni namna gani timu hiyo itampa nafasi.
Arsenal wamtolea macho kiungo wa PSG
LONDON, ENGLAND
KLABU ya Arsenal, nchini Uingereza ambayo kwa sasa ipo katika mbio za ubingwa inaarifiwa kwamba wanaweza kunasa saini ya nyota wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti.
Inaelezwa ikiwa itafanikiwa kumnasa kiungo huyo wa kati aliyezaliwa Septemba 5 1992 ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Italia itakuwa imeimarisha vema eneo la kati.
Pia mchezaji huyo ambae amekipiga katika kikosi cha PSG kwa msimu wa 11 , taarifa nyingine zinasema kama ‘deal’ la kutua Arsenal halitakwensa sawa uenda akarejea nchini kwao Italia.