ISTANBUL, UTURUKI
MWANASOKA mkongwe aliyekipiga kwenye klabu kadhaa kubwa barani Ulaya, Mesut Özil, ametangaza kustaafu kucheza mpira.
Özil mwenye umri wa miaka 34 ametangaza kustaafu leo Jumatano, Machi 22, 2023 kwa kuandika barua kwa mashabiki wake aliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya tafakuri ya kina, ninatangaza kwa grafla kawa ninastaafu kucheza mpira wa kulipwa. Nimebahatika kuwa mchezaji wa kulipwa kwa takribani miaka 17 na ninashukuru kwa upendeleo huo. Kwa wiki na miezi ya hivi karibuni nimekuwa nasumbuliwa na majeraha ambayo yamenipelekea kuchukua maamuzi haya.
Imekuwa ni safari ya kustaajabisha iliyojaa matukio yasiyosahaulika. Napenda kuvishukuru vilabu vyangu vya Schalke 04 (Ujerumani), Werder Bremen (Ujerumani), Real Madrid (Hispania), Arsenal FC (Uingereza), Fenerbahçe na Basaksehir (Uturuki) bila kuwasahau makocha walioniamini na kunipa nafasi ya kucheza, wachezaji wenzangu ambao wamekuwa marafiki wangu.
shukrani za kipekee ziende watu wa familia yangu na marafiki wa karibu maana wamekuwa sehemu ya safari yangu tangu siku ya kwanza na wamenipa mapenzi yaliyotukuka na msaada kwenye nyakati zote za dhiki na faraja.
Asanteni sana mashabiki wangu mlionionyesha mapenzi ya dhati bila kuangalia nyakati nilizopitia kenye vilabu vyote nilivyopita. Sasa naangalia mbele na kuanza maisha mapya nje ya soka nikiwa na mke wangu Amine na mabinti zangu wawili Eda na Ela lakini niwahakikishie mtaendelea kunisikia kwenye mitandao ya jamii,” ilisema taarifa hiyo ya Mesut Özil