LONDON, UINGEREZA
REAL Madrid wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 22, msimu wa joto kama sehemu ya mpango wa kuleta kizazi kipya cha nyota wachanga ambao pia ni pamoja na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 19. (Independent).
PSG KUMNG’OA MAGUIRE
BEKI wa Manchester United ambaye ni raia wa Uingereza, Harry Maguire, 30, amewekewa dau la pauni milioni 50 na Paris St-Germain msimu wa joto. (Sun)
MAN U YAMTUPIA JICHO MOUNT
KLABU ya ‘Mashetani Wekundu’ Manchester United imeongeza jina la kiungo wa kati wa timu ya soka ya Chelsea, Mason Mount, katika orodha yao ya usajili katika majira ya joto kwa lengo la kuhakikisha wanaimarimasha safu yao ya eneo la kati.
Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia ni raia wa Uingereza kwa sasa bado haijathibishwa kama atakubali kuijiunga na Mashetani hao Wekundu.