NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BAADA ya kuonekana kusuasua kwa kikosi cha Yanga Princes kwenye ligi kwenye Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, kocha wa kikosi hicho Sebastian Nkoma ameweka wazi kuwa haoni nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu.
Kocha huyo alibanisha hayo jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Fountain Gate uliochezwa kwenye dimba la Jamhuri jijini Dodoma na kukubali kipigo cha bao 1-0.
“Huo ndio ukweli hakuna sababu ya kusema tofauti na sababu kubwa wachezaji nilionao niliwakuta tayari wapo kikosini hivyo hakuna sababu ya kuwalaumu kikubwa ni kujipanga kuhakikisha tunamaliza katika nafasi nzuri,” amesema.
Kikosi hicho cha Yanga Princes hadi sasa kinashika nafasi ya nne kikiongozwa na Simba Queens yenye alama 23, ya pili ni Fountaine Gate yenye alama 23 mkononi ikitofautiana mabao ya kufunga na Simba na inayoshika nafasi ya tatu ni JKT Queens yenye alama 21 kibindoni na timu zote zikiwa katika mzungumko wa 10.