NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KOCHA wa timu ya Geita Gold, Fred Minziro, ametanabaisha kwamba wachezaji 22 ambao wamekuja nao Dar es Salaam wako ‘fiti’ kwa ajili ya kuajindaa na mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili Machi 12, 2023 kwenye dimba la Azam Complex .
“Wachezaji wangu wako fiti na niliowaacha baadhi yao wanachangamoto za kiafya, hivyo naamini waliopo watawawakilisha vizuri wenzao kwa kupambani kiwanjani na kupata alama tatu muhimu.
“Nafahamu Yanga inapambana kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na sisi tunapambana ili kukaa katika nafasi za juu katika msimamo na kutokana na mahitaji ya kila timu, naamini mchezo hautakuwa rahisi kikubwa naomba Mungu vijana wangu waamke salama siku ya mchezo na tushinde mtanange huo, amesema.
Kikosi hicho kilifika Machi 9, 2023 jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na leo Ijumaa Machi 10, 2023 wanafanya mazoezi yao katika dimba la Uhuru.