NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa klabu ya Vipers FC ya nchini Uganda inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) amefukuzwa kazi Kocha Mkuu wa timu hiyo Roberto Luiz raia wa Brazil huku kisa kikielezwa ni kufanya vibaya katika michezo ambayo imeshacheza ikiwamo ya dhidi ya Simba.
Katika michezo miwili ya CAFCL ya nyumbani na ugenini dhidi ya Simba ilipoteza kwa bao moja kila mchezo huku ikifungwa mabao 3-0 dhidi ya Raja na ikatoa sare dhidi ya Horoya FC wakiwa nyumbani na kwa sasa inashika mkia ikiwa na alama mbili mkononi.
Kutokana na matokeo hayo kwa sasa haina matumaini ya kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika na kuamua kuchukua jukumu la kumuondosha ili kutafuta kocha mwingine kwa ajili ya kujipanga na hatua nyingine.
Kocha Luiz, alichukua nafasi ya kocha wa sasa wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na amedumu kwa siku 58 tangu aijiunge na kikosi hicho pia licha ya kutofanya vema kwenye michuano ya Klabu BingwaAfrika pia hajafanya vema katika ligi ya ndani.