NA BARAKA JUMA, GEITA
WATU 10 akiwemo Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya IPP Media Richard Makore wamepoteza maisha na wengine 49 kujeruhiwa baada ya basi la Sheraton walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi , kuacha njia na kutumbukia kwenye daraja mkoani hapa.
Akithibitisha taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Sophia Jongo amesema ajali imetokea Jumanne Machi 07, 2023 saa 10 jioni maeneo ya Ibanda kona Kata ya Kasamwa wakati basi hilo likitokea Mwanza kwenda Ushirombo.
Kamanda Jongo amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi ambapo dereva alishindwa kumudu gari hilo na kutumbukia darajani
“Majeruhi na watu hao saba waliofariki wamehifadhiwa katika Hospital ya mkoa wa Geita nitoe wito kwa watu wote wanaotumia vyombo vya moto wahakikishe wanatii sheria bila za barabarani shuruti ili kuepuka ajali” amesema Jongo.
Hata hivyo Kamanda Jongo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Pollsi kama watabaini kuwepo kwa uvunjifu wa sheria za usalama barabarani ikiwemo na mwendo kasi.
