Juventus mbioni kumuongeza mkataba Di Maria
Juventus tayari wako katika mazungumzo na Angel Di Maria juu ya kuongeza mkataba wake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa mchezaji huru ifikapo mwezi wa Juni na bado hajadondosha wino kwenye mkataba mpya na klabu hiyo.
Di Maria (35) ambaye ameshinda kombe la dunia na Argentina, ameifungia magoli saba na kutengeneza nafasi saba zaidi katika michezo 23 toka ajiunge na Juve mwishoni mwa majira ya joto baada ya kumalizika kwa makataba wake na klabu ya Paris Saint-German. (Goal)
Roberto Firmino mbioni kuondoka Liverpool
IMERIPOTIWA kuwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Roberto Firmino huenda akaondoka katika klabu hiyo baada ya kuwaniwa na vilabu viwili kupata saini yake majira haya ya joto.
Taarifa zaidi zinasema klabu moja ambayo bado haijafahamika ya nchini Saudi Arabia inajiandaa kwa ofa kubwa kujaribu kumvutia Firmino kuhamia Mashariki ya Kati. (Football Insider)